YOBO ASILIMIA 80 NA SANGULA ASILIMIA 100 KUKOSA MCHEZO DHIDI YA KIPANGA

Wakati timu yetu ikitarajiwa kucheza mchezo wake muhimu leo dhidi ya Kipanga FC, mchezo ambao utakamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Zanzibar kanda A, yaani kanda ya Unguja kuna taarifa za uhakika za kutowatumia walinzi wote wawili wa kati wa kikosi cha kwanza na badala yake kutumika walizi wa akiba katika nafasi hio.

Nahodha Ibrahim Mohammed (Sangula) yeye ataukosa mchezo huo kwa sababu aliumia kifundo cha mguu mazoezini siku ya juzi (Ankle).



"Ni kweli Nahodha Sangula hatatumika katika mchezo wa leo dhidi ya Kipanga kwa sababu moja ni kwamba ameumia 'Ankle' mazoezini hili sote tunalifahamu" alisema katibu Dalas.

Kwa upande mwengine katibu alisema kwamba pia beki mwengine wa katikati wa kikosi cha kwanza hatatumika kutokana na kuumia "ankle" katika mchezo dhidi ya Mafunzo uliochezwa tarehe 27 Januari 2018 ambapo matokeo yalikuwa 1-1.

"Mbali ya Sangula, beki wetu mwengine Firdaus Seif maarufu Yobo pia na yeye tuna 'ati' 'ati' ya kucheza, alipatiwa dawa na madaktari lakini hadi sasa pamoja na kutumia dawa lakini bado daktari hajathibitisha kwamba anaweza kutumika, hivyo hakuna uhakika hadi sasa wa yeye kucheza, hivyo tutamia mabeki wa akiba.

"Fomu yetu ya usajili ina wachezaji 30 na wote hawa wanahudhuria mazoezi na wanafanya mazoezi mamoja, hii ni kusema kwamba hata hawa wa akiba wana uwezo wa kuziba mapengo ya hao wa kikosi cha kwanza, sisi viongozi tunawaamini sana, hivyo niwasihi washabiki na wao wawaamini" alimaliza Dalas.

Mbali ya wachezaji hao pia mshambuliaji Hassan Banda pia hatakuwemo kikosini humo kwa sababu bado anauguza bega aliloumia katika mchezo dhidi ya Mafunzo, halikadhalika Khamis Mussa (Rais) ataendelea kutooneka kiwanjani kutokana na matatizo yake binafsi.

Ikumbukwe huu ni mchezo huu ni muhimu sana kwa timu yetu, kwani endapo matokeo yakitupa fursa ya kuondoka na alama tatu timu yetu itakuwa imepiga hatua moja muhimu ya kusogea juu ya msimamo.

Dua zenu muhimu sana katika mchezo huu.

Maoni