ABDI KASSIM 'BABI' AITAKA MECHI DHIDI YA CHARAWE LEO

Kiungo wa Jang'ombe Boys mwenye uzoefu wa hali ya juu kushinda mchezaji yeyote ambaye anacheza ligi kuu kwa msimu huu wa 2017/18 Abdi Kassim 'Babi' au 'Balack' wa Zanzibar kama alivyomwita mchambuzi Edo Kumwembe amesema anaitamani na anaitaka sana mechi dhidi ya Charawe ambayo itachezwa leo baadae katika dimba la uwanja wa Aman.



Akizungumza baada ya kumaliza mazoezi ya mwisho ya timu hio na katika kuwajenga hamasa na kuonyesha umuhimu wa mchezo huo, 'Babi' alimuomba kocha Issa Othman (Amasha) kumpanga katika mchezo huo ili kuisaidia timu katika kupata ushindi na kukaa katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi ambayo imeonekana kuwa na ushindani wa hali ya juu.

"Tunakwenda kucheza mchezo na Charawe, Charawe ambao hawana matumaini ya kitu chochote, lakini tukumbuke Charawe anatafuta wa kufa nae, pia sasa hivi Charawe hachezi peke yake kuna walio juu yetu hao ni Charawe, pia kuna wa chini yetu pia ni Charawe hivyo tunakwenda kupambana vita kali sana.

"Katika mechi hii tunatakiwa kushinda magoli mengi sana, kiukweli hii mechi mimi naitaka sana, hivyo namuomba kocha Aamasha anipange katika mechi hii, kocha kwa hisani yako na kwa umuhimu wa mechi hii naomba usiweke nje" alisema 'Babi'.

Kwa niaba ya mtandao huu tunaiombea timu yetu mchezo mwema, salama na wa ushindi mnono.



Maoni