FINI AFURAHIA KUIMARIKA KWA KIWANGO CHAKE

Kiungo mshambuliaji wa Jang'ombe Boys Helfini Salum amesema anafurahia kuona kwamba kiwango chake kinaboreka siku hadi siku akiwa na Jang'ombe Boys.

Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kumalika kwa mchezo dhidi ya Charawe FC, mchezo ambao ulikuuliku
wa mzuri na wa kuvutia, huku vijana wetu wakionekana kumiliki mpira kwa kipindi vyote viwili vya mchezo.

"Ni kweli naonekana kuimarika sasa kwa sababu kila mechi nimekuwa nikifunga magoli sasa, na hili ndio lengo letu sisi wachezaji ili kunipa furaha na heshima timu yetu.

" Lakini niseme haya yamekuja baada ya kuanzia kuyazoea mazingira ya timu sambamba na aina ya uchezaji ambao Mwalimu alitaka nicheze.

"Binafsi nimefurahishwa na kiwango Changu na nawambia washabiki wawe na matumaini mema juu yetu kwani mazuri zaidi ya hay tutawafanyia, hivyo waendelee kuipenda timu yao kwa hali na mali" alimalizia Helfeni Salum.

Katika mchezo huo ulioonekana mgumu mwanzoni, Jang'ombe Boys imepata ushindi muhimu kwa kuifunga Charawe 2-0 Helfini Salum aliifungia timu yake goli la pili katika dakika ya 74 na goli la kwanza lilifungwa mshambuliaji Muhamadi Soud (Makamo wa Rais) katika dakika ya 54 ya mchezo.

Mtandao huu unaipongeza timu nzima kwa kutuletea ushindi katika timu yetu.



Maoni