'FINI' AWASHANGAZA WACHAMBUZI NA WATANGAZAJI JUU AINA YA UCHEZAJI, KOCHA AMASHA AWEKA SAWA

Kiwango cha uchezaji kilichoimarika cha mchezaji Helfein Salum (Fini) sambamba na aina ya uchezaji, kinawashangaza baadhi ya watangazaji na wachambuzi wa mchezo wa mpira wa miguu, hilo limedhihirika juzi wakati timu yetu ilipocheza na timu ya Kilimani City na hatimae kutoa kipigo cha paka mwizi kwa kuifunga Kilimani City goli 3-1. ambapo kiungo wetu mshambuliaji alikuwa ndiye wa kwanza kuandika goli la kuongoza mnamo dakika ya 12 akipokea pasi safi kutoka kwa Mustafa Vuai.


Akifanya mahojiano baada ya mchezo huo mtangazaji wa Zanzibar Cable Television (ZCTV) alitaka kujuwa ni nafasi gani Fini anacheza na ni aina gani ya uchezaji ambao anatumia, kwa sababu amekuwa akionekana anashuka hadi nyuma na baadae anaonekana yuko mbele, huku akiwa na mwendo na uchezaji ule ule bila kuchoka.

Mtangazaji (Namala): Tumeshuhudia mfungaji wa goli la kwanza Helefein Salum,
watu wanajiuliza ni aina gani ya middle field anacheza, imekuwa hatumuelewi anaishi wapi kiuchezaji, kwenye kukaba yupo kwenye kushambulia yupo, mwalimu unaweza kutwambia ni aina gani unatumia?

Kocha Amasha: Ah Fini anakuwa  ni kiungo mshambuliaji.

Mtangazaji (Namala): Tumeona kwenye kukaba yupo kwenye kushambulia yupo mwalim.

Kocha Amasha: Aha unajuwa mpira wa kisasa (morden football) ndio unavotaka, timu ikishambuliwa viungo vinashuka na timu ikishambulia viungo vinapanda.

Kwa niaba ya mtandao huu tunampongeza Fini na wachezaji wote kwa viwango vya hali ya juu walivyoonyesha, yote hayo yamekuja kwa juhudi na kuhudhuria mazoezi vizuri, hivyo nawanasihi wazidishe bidii katika mazoezi ili wafanye vyema kwa faida yao lakini pia kwa timu yetu.




Maoni