JANGOMBE BOYS KUWEKA REKODI MPYA LEO DHIDI YA CHUONI FC.



Leo majira ya saa 10.15 za alaasiri Jang'ombe Boys tutaingia tena kiwanjani Amani kucheza mchezo muhimu sana kuwahi kutoka, umuhimu wa mchezo huu ni kwa mambo yafuatayo:

  • Kukaa katika nafasi nzuri. 
Ushindi katika mchezo wa leo, utatuondoa katika nafasi tulio sasa, yaani nafasi ya 10 na tunaweza kukwea hadi katika nafasi ya 5, 6, au7, kutegemea idadi ya magoli.
  • Kubadili historia ya timu hizi mbili.
Jang'ombe Boys huu ni msimu wake wa tatu tokea ipande daraja katika ngazi ya ligi kuu, lakini rekodi haiibebi timu yetu, bali inaibeba kidogo Chuoni.

Kwani katika mara tano timu hizo zilizokutana, Chuoni imewahi kutufunga mara moja kwa kutufunga mabao 4-3 na michezo minne iliyobakia yote tumetoka suluhu ya 1-1, 1-1, 1-1 na 0-0.

Hivyo ni kwamba sisi hatujawahi kuifunga Chuoni zaidi ya kupata suluhu, lakini wao wameshatufunga mara moja, ingawa katika Mara nne ambazo tumetoka suluhu lakini Picha ya ushindi huwa umetuelekea lakini lutokana na Chuoni kutoka kubakia na historia nzuri basi hukomaa na kukamia sana, kitu ambacho kinawasaidia kupata suluhu.

Lakini kutokana na muunganiko wa timu ulivyo sasa na kiwango kizuri cha wachezaji pamoja na ugumu wa mchezo huu, bado nabakia na matumaini chanya kwamba timu yetu itapata ushindi katika mchezo wa leo.

Na kwa ushindi huo tutakaa katika nafasi nzuri ya ligi na kupata matumaini ya kwenda juu zaidi ya msimamo katika michezo inayofuata.

Washabiki na wadau njoni mushuhudie mtanange huu wa kipimzani zaidi.

Maoni