NIMEANZA KUONJA LADHA YA LIGI KUU: 'MAKAMO WA RAIS'

Mshambuliaji Muhamadi Soud (Makamo wa Rais) asema sasa ameanza kuona furaha ya ligi kuu ya Zanzibar (ZPL), Muhamadi ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Charawe.


Akiongea mbele ya mtandao huu Muhamadi amesema michezo ya hivi karibuni imenza kumuonjesha furaha ya ligi kuu ya Zanzibar kwani, amekuwa akifunga magoli mfululizo sambamba na kutoa pasi za magoli.


"Sasa kidogo kidogo naanza kuionja furaha ya ligi kuu ya Zanzibar, kwani furaha ya mshambuliaji kwanza ni kufunga magoli na baadae kutoa pasi za magoli, sasa Haya yote nimekuwa nikiyafanya kwa sasa.

" Ni kweli mwanzoni sikuwa nikifunga, ingawa nikizisumbuwa beki za timu pinzani, hii ilitokana na ugeni wangu katika ligi kuu, pia aina ya uwanja nayo ilikuwa ni kikwazo chengine, lakini pia mfumo wa mwalimu, lakini kwa sasa yote hayo yametulia kichwani kwangu.

"Kiukweli naipenda timu yangu hii mpya kwa sababu nimepokelewa kwa uzuri, kuanzia wachezaji, washabiki, walimu na wadau wote wa timu hii, nimekuwa nikifarijika sana na hamasa ninayojengwa na watu mbali mbali wa timu hii, jambo ambao natumai siku moja nitafika malengo.

" Nawaahidi washabiki kwamba nitawafanyia mazuri zaidi, muhimu washikamane na timu you kwa dua kwa sababu mpira wa kwetu una mambo mengi sana, hivyo watuombee dua kila kila wakati ili tuwaletee furaha zaidi" alimalizia Muhamadi (Makamo wa Rais).

Muhamadi alipachika goli la kwanza katika dakika ya 54 baada ya kuunganisha krosi safi iliyochongwa kiustadi na beki ya kushoto Juma Ali Mohammed, na bila ya ajizi  akaunganisha krosi hio kwa Kichwa chenye kasi na kuutumbukiza wavuni huku akimuacha goli kipa wa Charawe akigaragara kama nyungunyungu.

Hadi mwisho Jang'ombe Boys 2-0 Charawe.

Maoni