'FINI' NA 'YOBO' WAIKWEZA J.BOYS HADI NAFASI YA TATU KATIKA MSIMAMO WA LIGI

Katika kile kilichotarajiwa na wachezaji, wana chama, washabiki na wadau wote wa Jang'ombe Boys katika mchezo wa jana dhidi ya timu ya Zimamoto ndicho kilichotokea.


Mpira ulianza kwa kasi huku vijana wetu wakionekana kucheza kwa kujiamini bila hofu ya aina yeyote dhidi ya timu ya Zimamoto, kitendo ambacho kiliwafanya wamiliki mpira kwa muda mwingi.

Ilimchukuwa dakika 24 pekee kupata goli la kuongoza kupitia kiungo wetu aliyeimarika vya kutosha na kuwafanya wachambuzi na wadau wa mpira wa Zanzibar washangae kwa jinsi anavyohaha kiwanjani bila kuchoka,  ni Helfeni Salum (fini) ambaye alipachika wavuni goli la kiufundi, goli ambalo lilidumu hadi dakika 82 ambapo Ali Salum (kibata) alipofunga goli kwa mkwaju wa masafa marefu ulimshimda mlinda mlango wetu Bakari Mshenga, goli ambalo lionyesha dalili za kutuchanganya.

Lakini ukicheza na Jang'ombe Boys usiamini hadi firimbi ipulizwe kuashiria mpira umemalizika, kwa sababu pamoja na kurejeshewa goli katika dakika mbaya, lakini makamanda wetu hawakuvunjika moyo waliendelea kuliandama lango la Zimamoto walioonekana kuwa na furaha baada ya kusawazisha goli, lakini mnamo dakika ya 89 na sekunde 50 tulipata kona, kona ambayo ilichongwa na mshambuliaji Mustafa Vuai (Tafa), ambapo ndipo hapo Firdaus Seif (Yobo), akaufanya uwanja wa Amani kurindima kwa vificho na mayowe ya furaha na pongezi.

Hadi mwisho Jang'ombe Boys 2 Zimamoto 1 na matokeo hayo moja kwa moja yameipeleka Jang'ombe Boys kushika nafasi ya tatu nyuma ya vinara JKU na KVZ ambao wote wana alama 39 wakiwa na michezo sawa.

Pongezi za dhati ziwaendeee Helfin Salum na Firdaus Seif (Yobo).

Maoni