ANGALIA 'VIDEO' YA GOLI LETU LILILOKATALIWA DHIDI YA ZIMAMOTO KATIKA MCHEZO WA MWANZO WA LIGI KUU MSIMU WA 2017/18 .

Tumebakiwa na Massa 19 kufikia mchezo wetu wa pili wa ligi kuu ya Zanzibar dhidi ya maafande wa Zimamoto.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mwanzo wa ligi kuu inayoendelea tulitoka sare tasa, yaani 0-0.

Katika mchezo huo tulibahatika kufunga goli, goli ambalo muamuzi alilikataa kwa madai ya kwamba mfungaji wa goli hilo 'Pina' alikuwa ameotea, kitendo ambacho kilizuwa masuali mengi kwa wapenzi wa mpira wa haki.

Lakini kwa kuwa katika mchezo wa mpira muamuzi kama lilivyo jina lake, yeye huwa ndio muwamuzi wa mwisho, hivyo tulihishimu maamuzi yale ingawa kwa maumivu makali sana.

Angalia video ya goli hilo.


Maoni