JANG'OMBE BOYS YASAFIRI KUCHEZA FAINALI YA KOMBE LA MUUNGANO LEO


Klabu ya Jang'ombe Boys imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya Kombe la Muungano, ambalo miaka mingi mashindano hayo yanayozishirikisha timu za Zanzibar na Tanganyika kuunda mashindano hayo yalikosa kufanyika.



Jangombe Boys imefanikiwa kutinga hatua hiyo ambapo baadae jioni ya leo wataumana na timu iliyopanda daraja la ligi kuu ya Vodacom msimu huu Mbagala Market FC kumpata bingwa wa kombe hilo, ambapo kabla ya Jang'ombe Boys kufika hatua hiyo walifanikiwa kuitoa timu ya Black sailors kwa mikwaju ya penati 4-2, na baada hapo jana wakaweza kuizaba kibao kimoja timu ya Kijichi FC.

Mchezo huo utasukumwa katika dimba la uwanja wa Bandari uliopo jijini Dar es salaam na timu yetu imewasili salama jijini Dar es Salaam kusubiria mchezo huo wa fainali.

Mtandao huu ulizungumza na katibu wa timu hiyo Abdalla Mafoudh (Dallas) ambaye yupo pamoja na kikosi hicho, katika mahojiano tulioyafanya katibu ameanika hadharani jumla ya wachezaji 19 na viongozi 6 ambao wamesafiri na timu hio.

Hawa ndio wachezaji ambao wamesafiri kwa ajili ya pambano hilo:

  1. Hasham Haroun
  2. Bakari Mshenga.
  3. Suleiman Ali (Pichori)
  4. Suleiman Haji (Dejong)
  5. Frdaus Seif (Yobo)
  6. Ibrahim Mohammed (Sangula)
  7. Salum Seif
  8. Salum Abdalla
  9. Mustafa Vuai (Tafa)
  10. Khelfeni Salum (Fini)
  11. Mansour Marzouk
  12. Juma Ali (messi)
  13. Mohamadi Soud (Makamo)
  14. Mohammed Haji (XBox)
  15. Khatibu Ameir 
  16. Hassan Seif (Banda)
  17. Rashid Mohammed (Chidi)
  18. Mohammed Kipande 
  19. Yakoub Amour
Viongozi waliosafiri na timu ni:
  1. Ali Othman 
  2. Abdalla Mahfoudh (Dalas)
  3. Kombo Khamis
  4. Issa Juma
  5. Uledi Ramadhan
  6. Nassir Kheri
Tunaiombea timu yetu mchezo mwema utakaozaa ushindi kwa timu yetu - Amiin.

Maoni