GOLI LA 'BABI' VS JKU LAFUFUA MATUMANI YA KUCHEZA NANE BORA

Naam,  ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu sana, kumaliza mchezo wetu dhidi ya JKU kwa salama na ushindi, haikuwa kazi rahisi kupata ushindi huu ambao ni ushindi wa machozi na damu, kila aliyekuepo kiwanjani alishuhudia jinsi tuanavyotoka jasho na kulia, na tunaowalilia hawajali machozi yetu wala jasho tunalomwaga kwa ajili ya timu yetu, lakini yote kwa yote tumeshinda na kujiweka katika matumaini mazuri.

Abdi Kassim 'Babi'

Tumewapiga JKU goli moja bila majibu, goli ambalo limewekwa kimiani na mkongwe Abdi Kassim (Babi), goli ambalo naweza kusema ni la msimu laiti ingalikuwa kuna uongozi bora katika soka letu wenye kufanya tathmini ya matukio mbali mbali ya mpira na mwishowe kuyatangaza, hii ingeleta hamasa na kuengeza thamani za wachezaji wetu, lakini yote yanahitaji wasimamizi makini wanaopokea ushauri na kuufanyia kazi.

Ushindi huu umeisogoza timu yetu katika nafasi ya 6 katika msimamo tukiwa na alama 39 ikiwa ni tafauti ya alama 7 na kinara KVZ, pia tofauti yetu na timu ya ilio katika nafasi ya pili ni alama 3, tafauti kati ya wanaoshika nafasi ya tatu na ya nne ni alama 2 na tafauti yetu na mshika nafasi ya 5 ni alama 1 pekee.

Hivyo kuna haja kuzidi kushikamana na kuungana ili tuweze kushinda michezo iliyobakia tukianzia wa tarehe 6 Mei 2018 dhidi ya Taifa ya Jang'ombe, ambapo mchezo huu hautakuwa mwepesi licha ya Taifa kuonekana kuboronga katika msimu huu, kwa sababu huu ni mchezo maalum ambao ni wa kiupinzani (Dabi).

Hivyo bado nasisitiza mshikamano wa hali na mali, ili kuujinasuwa na kukosa kuiona timu yetu ikishiriki nane bora, ambapo hadi sasa tupo katika foleni nzuri ya kulifanikisha hilo, lakini yote yanategemea mshikamano wetu kama timu.

WITO WA MCHEZO DHIDI YA TAIFA: TUSHIKAMANE ILI TUMFUNGE MKOMBOZI TUCHEZE NANE BORA

Maoni