RAIS WA TIMU YA JANG'OMBE BOYS AITISHA MKUTANO

Rais wa jang'ombe Boys Ali Othman (Kibichwa) ameitisha mkutano mkubwa ambao utawakutanisha wadau wote wa timu hio, wakiwemo viongozi, wanachama, washabiki na wapenzi wa timu mkutano huo utafanyika katika kiwanja cha Timu hio mnamo Jumatatu ya tarehe 27/08/2018 saa kumi za alasiri.

Ali Othman (Kibichwa) akihojiwa
na waandishi wa Habari.

Akizungumza na mtandao huu Kibichwa amesema lengo la mkutano huu ni kujadili mambo mbali mbali yanayohusu timu yetu, yakiwemo usajili, uhamisho na mambo mengineyo.

"Kwa kuwa mwaka huu tumejipanga kivyengine, yaani ile dhamira hasa ya kuwa mabingwa wa ligi kuu mwaka huu ndio utekelezaji wake, kwa sababu tumeshaisoma ligi kwa miaka mitatu, fitna zote za ligi tumeshazisoma, hivyo sasa tunasema inatosha kuwa washindi wa tatu na zaidi, sasa ni mwendo wa ubingwa.

"Kwa hivyo basi ndio maana nikawaona ni vyema niwaite wadau wahusika wa timu wote, ili waje wajuwe hasa nini matarajio ya msimu huu, na mbinu zitakazotumika kuyatimiza matarajio hayo, pia siku hio kamati ya usajili itakuja na majina ya wachezaji wapya ambao tayari tumeshakubaliana nao, smbamba na kuwatangazia wachezaji ambao klabu itaachana nao, hivyo wadau wote wa timu yetu nawaomba siku ya tarehe 27/08/2018 mufike kwa wingi sana, ili kuja kujuwa mwelekeo na msimamo wa timu yenu msimu wa 2018/19" alimalizia Rais Ali Othman.

Kwa mujibu wa taarifa za chini chini zilizonyukwa na mtandao huu, ni kwamba mwaka huu Jang'ombe Boys watakuwa na kikosi khatari hakijawahi kutokea, wakijumuishwa wachezaji makinda wenye vipaji ambao hawajawahi kuonekana katika ligi kuu, shime muje kwa wingi na kwa wakati.

Maoni